Mwanamuziki nyota wa hip hop Bongo, Fid Q amesema bado anaamini alichofanya Diamond katika ngoma yake ‘Fresh Remix’ ni sahihi licha ya kukosolewa vikali.

Fid Q amesema kuwa alichofanya muimbaji huyo ni kueleza hisia zake na wala hajageuza hip hop kuwa taarab kama wengi wanavyodai baada ya kutoka kwa ngoma.

Amesema kuwa “Kwenye hip hop ukishapanga kufanya kolabo na mtu na mmeshapanga inatoka hata kama kakuchana inabidi uitoe, kufuta mstari wa mtu ni kosa,”.

Pia ameendelea kusema kuwa “Kwa hiyo bado nasisitiza alichofanya Baba Tiffah kwenye Fresh ni kitu sahihi kwa sababu zile ni hisia zake za maisha yake ya kila siku, ni kitu sahihihi wala siyo taarabu,”.

Mwana hip hop huyo ameongeza kwa kusema kuwa si kweli amefanya hip hop kuwa taarab bali taarab ndio inakopi hip hop ambayo ni kubwa zaidi ya maisha yenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *