Mkali wa hip hop nchini Fareed Kubanda “Fid Q’  amewafungukia na kuwachana baadhi ya watu wanaowabeza wasanii wa singeli, Man Fongo na Sholo Mwamba.

Fid Q amesema kuwa wanamuziki hao wameleta impact kubwa kwa jamii kwa hiyo kuwabeza ni sawa na kuikosea kabisa tasnia nzima ya muziki wa bongo kwasasa.

Man Fongo
Man Fongo

Rapa huyo mkongwe amsema kuwa Man Fongo na Sholo Mwamba wameleta mapinduzi ya muziki wa kizazi kipya.

Aliongeza kwa kusema kuwa unapomuongelea Man Fongo unaongelea mapinduzi ya muziki mpya wa kizazi cha sasa cha bongo kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki huo.

Sholo Mwamba
Sholo Mwamba

Pia Fid amesema kuwa Man Fongo ndiye mfalme wao pamoja na Sholo Mwamba katika muziki huo kutoka na kupokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wa singeli ambao umeonekana kufanya vizuri kwasasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *