Staa wa hip hop Bongo, Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amedai idadi ya views katika mtandao wa YouTube si kipimo kwa wasanii wa hip hop nchini.

Fid Q amesema kuwa idadi ya viewers mara myimgi huenda kinyume na uhalisia wa mapokeo ya wimbo wa msanii kutokana na idadi.

Mkali huyo wa hip hop amefunguka kwa kusema kuwa “Kwanza nafikiri nyingi hazipati (views) hizo kwa sababu wana hip hop ni watu ambao huwa tunatoa ngoma na zinakuwa zimefika.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Unajua views na mambo ya YouTube sometimes hayamati sana katika uhalisia, huwa tunakutana na watu ambao wana-views milioni na kadhalika katika show na tunakuwa kama sisi ndio tuna hizi views milioni,”.

Ameongeza kwa kusema kuwa  “Kwa hiyo huwa nawaambia watu kila siku kwamba number do lie sometime, kwa sababu unaambia mbili jumlisha mbili ni nne na mbili mara mbili ni nne lakini mbili toa mbili ni sifuri,”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *