Mkurugenzi wa Yamoto Band Said Fella amesema kuwa muziki wa taarabu haujakufa kama baadhi ya watu wanavyosema ila mashabiki wanataka muziki mzuri kutoka kwa wasanaii wa muziki huo.
Said Fella ambaye ameingia kwenye muziki wa taarab kwa kuanzisha bendi ya ‘Yah TMK Taarab’ amedai hakuna ukweli wowote kwamba muziki wa taarab umekufa.
Amesema kuwa “Mimi siamini kwamba muziki wa taarab umekufa, mashabiki wapo wanazaliwa kila siku wanataka muziki mzuri.
Fella amesema yeye pamoja na bendi yake hiyo wamejipanga kuleta ushindani mpya kwenye muziki wa bendi kwa kuachia kazi nzuri.
Bendi hiyo ya Fella inaundwa na wasanii nyota wa muziki huo waliotamba katika bendi mbali mbali za taarabu nchini akiwemo Omar Tego na Maua Tego waliokuwa Coast Modern Taarab na Fatuma Nyoro kutoka Jahazi Modern Taarab.