Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae Foundation pamoja na Yamoto Band, Said Fella amesema anatarajia kumuachia Temba kuwasimamia kundi la Yamoto Band pamoja na Foundation ya Mkubwa na Wanawe.

Fella amesema tayari ameshampata mtu sahihi ambaye atamwachia mikoba yake ya kusimamia wasanii pale atakapostaafu muziki.

Fella amesema atamwachia kijiti Temba na tayari ameshamuandaa vya kutosha na bado anaendelea kumuandaa zaidi huku akisema akisisitiza kwamba Temba tayari anaelewa nini anatakiwa kufanya muda ukifika.

Temba
Temba

Kwa upande wa Temba amesema yupo tayari kupokea majukumu atayoachiwa na bossi wake huyo.

Pia Temba alisema hata kama akiwa kwenye jukumu la umeneja hataacha kufanya muziki kwa kuwa muziki ni sehemu ya maisha yake.

Temba ni mwanamuziki anayeunda kundi la TMK Wanaume Family akiwa na Chege ambalo pia lipo chini ya Mkubwa Fella.

Temba ni msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini ambaye ameanza muziki miaka ya tisini ambapo anaendelea kufanya muziki hadai sasa anapotarajiwa kukabidhiwa kijiti cha umeneja katika Foundation ya Mkubwa na Wanawe.

Temba aliwahi kutamba na nyimbo kibao zilizokonga nyoyo za mashabiki wa Bongo fleva kama, Nampenda yeye aliyemshirikisha Dully Sykes pamoja Side Myamwezi na zingine nyingi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *