Mkurugenzi wa Yamoto Band, Said Fella amesema Yamoto Band haijafa kama watu wanavyodhania bali walikuwa wanafanya tathmini katika kazi zao walizokuwa wamezifanya tangu walivyoanza muziki.

Fela amesema hayo baada ya kundi hilo kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo zaidi ya miezi sita sasa huku wadau wakidai uhenda kundi hilo limekufa.

Hayo yameibuka baada ya ukimya wa takribani miezi saba kwa kikundi hicho bila ya kutoa kazi mpya ya aina yoyote wala kuonekana katika viwanja mbalimbali vya sanaa ndani ya Tanzania.

“Siyo kila siku kwamba utatoa ngoma mpya, unatakiwa muda mwingine utafute hela ya zile ngoma ulizozitoa na kikubwa mwanzo huwa unatafuta ukubwa kisha ukishapata unaanza kutoa ngoma taratibu taratibu siyo kila siku, wiki hata mwezi unataka kutoa ngoma unashinda na nani?, uzuri wa Yamoto wamezaliwa kwa mtu anayejua muziki vizuri hivyo siasa zote nazijua katika sanaa kwa hiyo lazima tupange mipango ya kwenda na kuangalia mashabiki kama tunao”. 

Pia Fela ameweka wazi mipango ya kundi hilo na kusema siku ya Ijumaa wanatarajia kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Basi’ ambayo itakuwa inawarudisha tena watoto hao katika ulimwengu wa muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *