Mkurugenzi wa Yamoto Band ambaye ni Diwani wa kata ya Kilungule, Said Fella amepokea msaada wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia kwa shule za msinigi na sekondari kutoka Oxford University Press Tanzania.

Msaada huo wa vitabu umegaiwa katika Shule za msingi Chalambe, Chemchem na Kingugi kwa upande wa shule ya sekondari umekwenda kwa shule ya sekondari Chalambe nje kidogo ya mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya kupokea msaada huo Fella amewashukuru Oxford kwa msaada huo huku akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuvitunza vitabu hivyo ili wadogo zao waje kuvisoma siku za usoni.

Said Fella akiwa wawakilishi wa Oxford, walimu na wanafunzi wa shule waliopewa vitabu hivyo.
Said Fella akiwa na wawakilishi wa Oxford, walimu na wanafunzi wa shule waliopewa vitabu hivyo.

Pia Fella amewaomba wadau mbali mbali kuiga mfano wa Oxford kuisaidia kata hiyo mpya ya Kilungule kwani inachangamoto nyingi kutokana na upya wake.

Kwa upande wa mwakilishi wa Oxford Maria Mlaya amesisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kupitia vitabu hivyo ili kutimiza ndoto zao katika maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *