Mkurugenzi wa Yamoto Band, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amekanusha tetesi zilizosambaa kuwa ana bifu na mwanamuziki Diamond Platnumz huku akisema habari hizo si kweli.

Tetesi za bifu la wawili hao zinasema kuwa wasanii wa Bendi ya Yamoto anayoisimamia kumlalamikia Diamond ambaye pia ana hisa kwenye bendi hiyo kwamba mkurugenzi wao huyo anawanyonya na kazi zote wanazopiga wao wanamnufaisha yeye tu.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz

Fella amesema kuwa hakuna kitu kama hicho na haijawahi kutokea kabisa, hayo ni maneno tu ya watu na wala yeye na Diamond hawajawahi kuzungumza kitu kama hicho.

Fella na Babu Tale ni mingoni mwa maneja wanaommiliki Diamond lakini kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na tofauti kutokana na Fella kutoshiriki sana mambo ya WCB mpaka watu wakaanza kuwa na wasi wasi uhenda kuna tofauti kati ya wawili hao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *