Klabu ya Fenerbehce ya Uturuki imeonyesha nia ya kumsajili mshambulizi Mbwana Samatta KRC Genk ya Ubelgiji.

Kwa sasa, mkongwe Robon van Persie ndiye kiongozi wa ushambulizi katika timu hiyo ya pili kwa ukubwa nchini Uturuki baada ya Galatasaray.

Lakini  Fenerbehce  inaonekana imeamua kujiimarisha na sasa inasaka mshambulizi kijana na hatari, Samatta anatupiwa jicho.

Wengine ambao wanapewa nafasi ya kusajiliwa na Fenerbehce  ni Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *