Shirika la Ujasusi nchini Marekani (FBI) limesema kuwa mgombea urais kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton hana shitaka la kujibu baada ya kupitia barua pepe zake na kujiridhisha.

Mkurugenzi wa FBI, James Comey ameliambia bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia barua pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton wakati alipokua waziri wa mambo ya nje wamegundua kuwa hana hatia yoyote na hawatamfungulia mashtaka.

Kampeni za Clinton ziliingia doa wiki iliyopita baada ya mkurugenzi huyo wa FBI kusema kuwa watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika kompyuta ya msidizi wa zamani wa mume wake.

Kauli hiyo imeonekana kumfurahisha mkuu wa mawasiliano wa kampeni za Clinton Jennifer Palmieri.

Wakati upande wa Bi Clinton wakifurahia hatua hiyo kwa upande lakini imekuwa tofauti upande wa mpinzani wake Donald Trump amesema Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa kura huku akisema Bi Clinton angetakiwa kuchunguzwa kwa muda mrefu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *