Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI limeanza kukusanya taarifa za uchunguzi wa muigizaji wa Hollywood, Brad Pitt kuhusu watoto wake sita baada ya kukodi ndege binafsi.

Shirika hilo linaangazia uwezekano wa kuanzisha uchunguzi au la.

Mke wa Pitt ambaye ni Angelina Jolie anataka talaka kutoka kwa muwewe huo kutokana na kile alichokitaja kuwa tofauti zisizotatulika.

Jolie ametaka apewe watoto wote sita huku akimtaka jaji ampatie haki za kuwatembelea watoto hao mumewe.

Shirika hilo la ujajusi limeanza kufuatia madai yaliotolewa kuhusu ndege iliokuwa ikimbeba Pitt na wanawe , FBI linaendelea kukusanya ukweli na litaamua iwapo litaanza uchunguzi au la.

Pitt alitoa taarifa katika gazeti la People baada ya Jolie kuwasilisha ombi la kutaka talaka akisema ameshtushwa na hatua hiyo na kuongezea: kitu muhimu ni maisha mazuri ya watoto wetu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *