Lebo ya Roc Nation ya mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Jay Z imemsainisha rapa mkongwe Fat Joe kwa ajili ya kusimamia kazi zake za kumuziki.

Kwa mujibu wa Roc Nation album yake na Remy Ma, Plata o Plomo itakuwa ya kwanza kutoka akiwa chini ya label hiyo.

fat-joe-bryson

Fat Joe ni rapa mkongwe aliyeanza kufanya kazi miaka ya 1990 na kupata umaarufu kupitia vibao vyake vilivyokuwa bora miaka ya nyuma.

Albam ya mkali huyo ‘Plata o Plomo’ inatarajiwa kuingia sokoni Februari 17 mwaka huu baada ya kukamilika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *