Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imefunguka na kutoa msimamo wake kuhusu jeshi la polisi kwenye upelelezi wa Tundu Lissu.

Familia hiyo imesema kuwa hawaoni jitihada zozote kutoka kwenye jeshi hilo kuchunguza jaribio la mauaji ambalo ndugu yao lilimpata Septemba 7, 2017.

Mdogo wa Tundu Lissu ambaye anafahamika kwa jina la Vicent Mughwai Lissu amesema kuwa wanaona jeshi la polisi halipo ‘serious’ katika kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Lissu.

Aidha familia hiyo imelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi haraka juu ya sakata la ndugu yao kupigwa risasi na pia wamewaomba Watanzania waendelee kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona.

Mbunge Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *