Familia ya Gurdiola yanusurika katika tukio la kigaidi la Manchester

0
384

Familia ya Kocha wa Manchester City, Pep Guadiola ni miongoni mwa watu walionusurika na tukio la ugaidi katika Ukumbi wa Ariana Grand jijini Manchester.

Familia ya kocha huyo ilikuwepo wakati shambulio hilo likitokea tukio ambalo limestua dunia na kuchukuliwa kama tukio la kigaidi ndani ya jiji la Manchester.

Katika tamasha hilo mke wa Gurdiola aliambatana na watoto wake wawili wa kike lakini wote wamenusurika kwenye tukio hilo.

Pia inaelezwa kuwa baadhi ya wachezaji wa Manchester City ambao hawakutajwa majina yao walikuwepo na familia zao lakini hawakuathiriwa na shambulizi hilo.

Mkutano wa klabu ya Manchester United na vyombo vya habari kuhusu mechi yao ya leo umeahirishwa hapoa jana kutokana na tukio hilo lakin uongozi ukisisitiza kwamba mechi hiyo ipo kama kawaida.

Shambulizi hilo limetokea usiku wa kumkia jana katika jiji la Manchester nchini Uingereza na kusababisha vifo vya watu 22 na majeruhi 60 kwenye tukio hilo.

LEAVE A REPLY