Shirikisho la Soka nchini TFF limethibitisha kuwa mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho kati ya Simba na Mbao itafanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi amethibitisha kwamba uwanja utakaotumiwa kwenye fainali utakuwa ni Jamhuri mkoani Dodoma.

Malinzi amesema kuwa awali ilitakiwa kufanyika droo live ya kuchagua uwanja kutokana na vilabu vilivyoingia fainali vinatokea sehemu mbili tofauti.

Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

 “Kweli ni Jamhuri, awali ilikuwa ni droo lakini sasa moja kwa moja tumetangaza uwanja utakaofanyika ni Jamhuri,”.

Pia Malinzi amesema kuwa sababu nyingine iliyofanya mechi hiyo kuchezwa mkoani Dodoma kutokana na ukarabati wa uwanja wa Taifa ambapo baada ya ligi kumalizika na uwanja utafungwa kupisha ujenzi huo.

Itakuwa mara kwanza kwa fainali hiyo kuchezwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma mara baada ya kombe hilo kuanzisha rasmi mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *