Uwanja wa Vicente Calderon unaotumiwa na Atletico Madrid umetangazwa kutumiwa kwenye fainali ya kombe la mfalme kati ya Barcelona na Alavaes Mei 27 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini Hispania (RFEF), limeutangaza uwanja huo kwa ajili ya faianli hiyo ya kombe la Mfalme.

Sababu ya kuchaguliwa kwa uwanja huo ni kwasababu unatosha kukidhi haja ya mashabiki 55,000 watakaopata nafasi ya kuushuhudia, huku wakiwa wameketi vitini.

Mchezo huo wa fainali ya kombe la Mfalme utatoa heshima za mwisho kwenye uwanja wa Vicente Calderon unaomilikiwa na klabu ya Atletico Madrid tangu mwaka 1966, kufuatia dhamira iliyowekwa na uongozi wa klabu hiyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *