Fahamu vipaumbele sita vya IGP, Simon Sirro

0
495

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ametaja mambo sita ambayo atahakikisha yanamalizika ndani ya utawala wake baada ya kupandishwa cheo na Rais Magufuli wiki iliyopita.

Kamanda Sirro amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza toka achaguliwe nafasi hiyo. Mambo sita aliyoongelea Sirro ni kama ifuatavyo

Matukio ya kujichukulia sheria mkononi

IGP Sirro ametoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja na badala yake wananchi wajenge tabia ya kuheshimu na kufuata sheria za nchi, kwani kwa kufanya hivyo watasaidia vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Makosa ya Bodaboda

Amesema amewaagiza makamanda wote wa mikoa kuwashughulikia wale wote wasiofuata sheria za usalama barabarani ama kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Vitendo vya rushwa

Sirro amesema kumekuwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji huduma za kipolisi, lakini pia baadhi ya wananchi kuwashawishi askari kupokea rushwa kama ngao ya kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa wamefanya makosa na kuwataka wote kuacha tabia hiyo.

Dawa za kulevya

Kamanda Sirro amesema kuwa  vita inakwenda vizuri na wataendelea kuisimamia na kuwataka wale ambao kipato chao kilikuwa ni dawa za kulevya kuachana na hiyo biashara, kwa kuwa mwisho itawafanya kuacha familia zao.

Mauaji ya askari Polisi

Akijibu maswali kuhusu mauaji ya askari polisi, alisema mauaji hayo ni ajali kazini kwa kuwa unapopambana na uhalifu kuna mawili askaria afe au jambazi afe na ndiyo sababu wameapa na wana wajibu wa kutumia nguvu ya kadri.

Waandishi kupigwa

Akizungumzia matukio ya waandishi kupigwa, alisema wote ni wabia, hivyo wakati mwingine matukio kama hayo hutokea kwa bahati mbaya na siyo sahihi kumpiga mwandishi.

 

LEAVE A REPLY