Kampuni ya mitandao ya kijamii duniani Facebook inatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”watch”.

Teknolojia hiyo imebuniwa ili kushindana na televisheni za kawaida pamoja na mitandao ya you tube,Netflix, twitter na snap chat.

Facebook inasema kwamba imewekeza mamilioni ya dola katika kuifanya huduma hiyo kupendwa zaidi.

Nayo Kampuni ya Disney jana ilitangaza kuwa kuanzia mwaka 2019, itafuta makubaliano kati yake na kampuni ya Neflix na kuunda huduma yake mpya ya video.

Facebook tayari ina vipindi kadha vikiwemo vya michezo, vya familia na vya televisheni ya National Geographic.

Watch itaanza kuonyeshwa nchini Marekani kabla ya maeneo mengine kuruhisiwa kutazama huduma hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *