Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, John Jackson maarufu kama ‘Fabolous’ amesema kuwa mwaka 2017 utakuwa wa neema kwake kwa hiyo wanamuziki wenzake nchini humo wajipange kwa kuwa anakuja kwa kishindo.

Mkali huyo huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu, amedai kuwa mwaka 2017 anatarajia kufanya makubwa katika muziki huo kutokana na kukaa kimya kwa muda mrefu.

Fabolous amesema kuwa “Nilikuwa kimya kwenye muziki lakini sikuwa kimya kwenye harakati za maisha yangu, nilikuwa nafanya vizuri kwenye kutafuta fedha, lakini sasa nataka kurudi kwenye muziki kwa ajili ya ushindani.

Mkali huyo ameongeza kwa kusema kuwa “Nimekuwa nikiwasilikiza kila siku wasanii wachanga ambao wanafanya vizuri kwa sasa kwenye Hip Hop, hivyo wajiandae nakuja, tangu nimekuwa kimya sijaona msanii ambaye amevaa viatu vyangu katika nafasi yangu, basi nakuja mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *