Chama cha soka nchini Uingereza, FA kimetupa  t-shirt 4,000 zilizokuwa zimepangwa kugawiwa kwa mashabiki kwenye mechi ya Uingereza na Malta sababu zilikuwa na nukuu ya kocha aliyetimuliwa, Sam Allardyce.

Sam Allardyce maarufu kama Big Sam mwenye umri wa miaka 61alikuwa akijiandaa na mechi na mechi October 8 lakini kibarua chake kiliota mbawa baada ya kashfa yake ya rushwa kuibuliwa.

FA ilitaka kuzitumia t-shirt hizo kama kumbukumbu ya mchezo wake wa kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia. Zilikuwa zimeandikwa ‘The journey starts with us all pulling together’ kauli ambayo Allardyce aliiongea siku ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *