Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amefungiwa michezo mitatu kufuatia adhabu iliyotolewa na chama cha soka nchini Uingereza FA.

Adhabu hiyo ni kutokana na kosa la kumpiga kiwiko Tyrone Mings wa Bournemouth katika mchezo wa jumamosi iliyopita ulioisha kwa sare ya 1-1.

Mechi ambazo atakosa Manchester United na Chelsea kwenye robo fainali ya kombe la FA, Middlesbrough na West Bromwich kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Zlatan anatarajia kurejea uwanja kwenye mechi ya nyumbani dhidi ya  Everton tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *