Kiungo wa klabu ya Machester United, Ander Herrera amefungiwa michezo miwili na Chama cha soka nchini Uingereza baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya kombe la FA dhidi ya Chelsea.

Kiungo huyo atakosa mechi mbili baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ya pili ndani ya msimu mmoja, kadi ya kwanza alioneshwa dhidi ya Burnley October mwaka jana.

ander

Baada ya kufungiwa mechi hizo sasa anaungana na Zlatan Ibrahimovic aliyefungiwa mechi 3 kwa kumpiga kiwiko Tyrone Mings wa AFC Bournemouth.

Mechi atakazokosa Herera ni Middlesbrough na West Brom lakini atakuwa na nafasi ya kuitumikia Man United katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League utakaochezwa alhamisi hii dhidi ya Rostov katika uwanja wa Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *