Manchester United leo itakuwa mgeni wa Blackburn kwenye mechi ya kombe la FA katika uwanja wa Ewood Park.

Manchester United wanaingia uwanjani katika mechi hiyo huku wakiwa na kumbu kumbu nzuri juu ya Blackburn baada ya kukutana miaka ya nyuma.

Manchester United imefika nafasi hiyo baada ya kuitoa Reading inayofundishwa na aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Jaap Stam.

Mechi kati ya timu hizo inatarajiwa kuanza kuanzia saa moja na robo kwa masaa ya Afrika Mashariki.

Mechi niyngine mbali na Manchester na Blackburn itakuwa kati ya Fulham na Tottenham itakayofanyika katika uwanja Craven Cottage.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *