Aliyekuwa mpenzi wa msanii wa Bongo Flava Linah Sanga, Nagar aka Nagarico amefunga ndoa wiki iliyopita.

LINAHNANAGARI

Nagar pia aliwahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Wema Sepetu. Alifunga ndoa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja tu kuwa la KHADIJA na kusema hataki mambo yake kwa sasa yawe hadharani kama awali.

“Nimekutana naye na nikaona anafaa kuwa mke ndio maana nimefanya maamuzi hayo, kuna marafiki wachache wa Linah wamenitumia sms za hongera,” Nagar aliiambia Fahamu TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *