Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlamgosi amesema kuwa mamlaka hiyo imeongoza bei bei ya umeme kwa asilimia 8.5.

Ngalamgosi amesema kuwa ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme nchini Tanesco ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Mkurugenzi huyo wa EWURA amesema baada ya kufanya uchambuzi wa kina, mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa
gharama za uzalishaji wake.

Kwa upande wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa   asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

Viwanda vidogo vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakuwa na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *