Klabu ya Everton imewasili Jijini Dar es Salam kwa ajili ya mechi na mabingwa wa kombe la SportPesa, klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

Kikosi hicho cha Everton kimepokelewa na waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe katika uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA).

Everton imeongozwa na mchezaji nyota Wayne Rooney pamoja na Davy Klaassen na Michael Keane ambao pia wamejiunga na klabu hiyo msimu huu.

rooney

Kikosi kamili cha Everton kilichotua leo ni Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen.

Mechi kati ya hizo timu mbili itafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho kuanzia saa kumi na moja jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *