Klabu ya Everton imemfukuza kocha wake Ronald Koeman baada ya jana kufungwa goli 5-2 na Arsenal katika uwanja wa Gurdson Park.

Baada ya kichapo hiko kutoka kwa Arsenal timu hiyo imeshuka mpaka nafasi ya 18 baada ya kushinda mechi mbili kati ya mechi 9 za ligi walizocheza hadi sasa.

Koeman amekuwa kocha wa tatu kufukuzwa kwenye ligi kuu Uingereza msimu huu baada ya Frank de Boer wa Crystal Palace na Craig Shakespeare wa Leicester.

Kocha huyo aliisadia Everton kushika nafasi ya saba msimu uliopita lakini msimu huu ameanza vibaya licha ya kutumia paundi milioni 140 kwa usajili.

Mmiliki wa Everton, Farhad Moshiri alimpa kocha huyo nafasi  baada ya kufungwa 1-0 na Burnley, lakini wakasuluhu na Brighton na kupoteza na Lyon kwenye Europa ligi na jana kufungwa 5-2 dhidi ya Arsenal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *