Aliyekuwa nyota wa timu ya soka ya Cameroon Samuel Eto’o huenda akahudumia kifungo cha miaka 10 jela baada ya waendesha mashtaka kumhusisha na kashfa ya kukwepa kulipa ushuru.

Kulingana na ripoti mchezaji huyo wa zamani wa Cameroon pamoja na mshauri wake Josep Maria Mesalles wameshtumiwa kwa kulinyima taifa la Uhispania Euro milioni 3.8 kutoka mwaka 2006 hadi 2009,wakati alipoichezea klabu ya Barcelona.

Kashfa inayomuandama Eto’o inashirikisha madai ya kuhamisha haki za matumizi ya picha yake katika kampuni za Uhispania na Hungary ili kukwepa kulipa kodi, katika mikataba iliodhinishwa kama vile makubaliano yake na kampuni ya jezi za michezo Puma.

Waendesha mashtaka waliwasilisha malalmishi dhidi ya mchezaji huyo ,lakini naye akatoa taarifa inayolaumu swala hilo kuwa ”uonevu na ushauri wa kifisadi”.

Eto’o ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Uturuki ya Club Antalayaspor,anaaminika kutolipa fedha alizodaiwa hatua ambayo imesababisha kuanzishwa kwa mashtaka hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *