Shirika la Ndege la ETIHAD limezindua rasmi sehemu ya kupumzika kwa daraja la kwanza na kati katika eneo la  Tom Bradley  katika uwanja wa kimataifa wa Los Angels.

Ujenzi huo umeendana na ubora na kiwango cha huduma zinazotolewa, ikiwa ni ahadi ya huduma bora kwa wateja wa madaraja ya kwanza na kati wanaotumia ndege ya Etihad ya EY170 Boeing kutoka Marekani Magharibi na ukanda wa pwanai na kitovu cha burudani.

Pamoja na sehemu yenye hadhi ya juu ya kupumzika ya Etihad iliyopo Washngton DC na New York, huduma hii ya kwanza Los Angles(LA) imewekwa ili kuonyesha ukarimu kwa Wamerakani, ni huduma ya kwanza katika ukanda wa  Marekani Magharibi.

Huduma zinazopatikana katika sehemu za mapumziko kwenye viwanja vya ndege vinavyohudumiwa na ndege za Etihad zimewekwa kuendana na utamaduni wa Kiarabu  unaopatikana kwenye utamaduni wa Abu Dhabi.

Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Martin Drew amesemakwamba ikiwa ndilo shirika linaloongoza kwa huduma za anga ulimwenguni, Etihad imeendelea kuboresha huduma, na kuwa kiongozi kwenye ubunifu wa huduma zake kwa wateja ndani ya ndege na wawapo sehemu ya kupandia ndege.

Sehemu hiyo ina hoteli yenye ubora pia yamewekwa mazingira ya kuwahudumia watu hata wakiwa wengi. Sehemu mpya ya mapumziko inamwezesha mteja kuwa huru, kuburudika na kufurahia huduma kutoka kwa watoa huduma  wa ndege  za Etihad wenye uzoefu wa kutosha.

Kuna sehemu nzuri yenye kukufanya ujisikie vizuri ikiwa na viti vya kukaa, sehemu ya kupata mlo, bar na eneo la kutazama runinga, sehemu ya kuoga, sehemu ya matumizi ya mtandao ikiwa na soketi za kutumia USB pamoja na chumba cha magazeti na majarida ya ndani na nje ya nchi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *