Shirika la ndege la Etihad limetangaza punguzo la bei katika safari zake duniani kote ikiwa ni njia mahususi ya kuwahamasisha watanzania kusafiri zaidi duniani.

 Ili kufurahia ofa hiyo mteja anatakiwa kupanga safari yake mapema na kujipatia tiketi yake mapema katika madaraja ya Biashara na Uchumi na mapumziko katika miji mbalimbali ya chaguo lako ikiwa ni pamoja  na Abu Dhabi, Dubai, London, Ahmedabad, New Delhi, Mumbai, Beijing, Hyderabad, Muscat na Paris.

 Bei maalum katika daraja la Uchumi zitapangwa rasmi kuanzia sasa na tarehe 31 Julai 2017 na mteja kuweza kusafiri kuanzia tarehe 17 Septemba hadi Mei 30 mwaka 2018.

 Kwa wale wanaotamani kujionea daraja la biashara la Shirika la Ndege la Etihad ambalo limetunukiwa tuzo lukuki pia litapatikana kwa kununua tiketi zao mapema  kuanzia sasa mpaka tarehe 31.07.2017 kwa ajili ya kusafiri tarehe 14.08.2018 hadi tarehe 30.05.2018.

 Wasafiri wanashauriwa kununua tiketi zao mapema kupitia Etihad.com au kwa kupitia kituo cha kupigia simu cha Etihad kinachofanya kazi masaa 24, vile vile kupitia mawakala wa usafiri kuhakikisha wanapata nafasi za kwenda kutembelea sehemu mbali mbali duniani kwa bei nafuu na za kipekee huku wakijipangia tarehe au muda wa kusafiri wao wenyewe.

 Wageni wanashauriwa kuandika mapema kupitia etihad.com au kituo cha simu cha Etihad Airways ’24/7, au kupitia wakala wa kusafiri ili kuhakikisha upatikanaji wa vituo vya ajabu katika bei bora na chaguo la kusafiri.

Mfano wa nauli za Etihad kipindi hiki cha ofa kwa Tanzania (Nauli zote zinategemea usafiri wa kurudi na zitahusisha kodi na makato yote)

Destination

Safari

Daraja la 2

Economy

US$

Daraja la kwanza (Business)

US$

   
Abu Dhabi / Dubai 382 2,362
London 858 2,174
Ahmedabad 563 1,493

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *