Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amesema kuwa tume ya kitaifa ya haki za Kibinadamu tayari inachunguza vifo vya watu nchini humo.

Mapema mwezi huu mjumbe maalum wa Muungano wa EU kuhusu haki za kibinadamu aliitaka Ethiopia kushirikiana na Umoja wa mataifa kuhusu suala hilo.

Bunge la nchi hiyo hivi majuzi liliongeza muda wa hali ya hatari iliyotangazwa mwezi Oktoba mwaka kwa miezi minne zaidi.

Waziri mkuu huyo ametetea hatua ya serikali yake kuongezea muda tangazo la hali ya hatari iliyotangazwa mwezi Oktoba mwaka jana,akidai hali hiyo ilihitajika ili kuweza kukabiliana na baadhi ya watu ambao bado wana nia ya kuleta ghasia.

Kuhusu uchunguzi wa vifo vya mamia ya Watu waziri Desalegn amesema ni lazima haki ipatikane kwa sababu kuna nia ya kushughulikia hilo ndani ya Serikali.

Amesema uchunguzi umefanywa na matokeo yake yatawekwa wazi.

Mwimbaji mashuhuri ambaye pia ni jaji Alesha Dixon alimwambia Sara kuwa hakubaliwi kuwa na talanta kama hii katika umri wake.

Majaji wengine wawili wakiwemo David Williams, Amanda Holden pia walimmiminia pongezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *