Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imemthibitisha rasmi Esther Bulaya (CHADEMA) kuwa mbunge halali wa jimbo la Bunda Mjini baada ya kushinda Rufaa ya aliyekuwa mgombea katika jimbo hilo, Stephen Wasira (CCM).

Stephen Wasira alifungua kesi mahakama kuu kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa Ester Bulaya kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Ester Bulaya alikuwa mbunge wa viti maalumu wa Bunda mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia CHADEMA na kugombea ubunge wa Bunda mjini kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu.

Mahakama hiyo imemthibitisha Ester Bulaya kuwa mshindi halali wa kiti cha ubunge wa jimbo hilo la Bunda mjini na kutupilia mbali madai yaliyofunguliwa na Stephen Wasira ambaye alishika nafasi mbali mbali za uwaziri katika serikali ya awamu ya nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *