Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Michael Essien leo ametangaza kujiunga rasmi na timu ya Persib Bandung ya Indonesia baada ya kuwa nje ya uwanja bila timu kwa miezi sita.

Essien alikuwa hana timu kwa kipindi cha miezi sita baada ya kuachana  na Panathinaikos ya Ugiriki mwaka 2016 na amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha akiba cha Chelsea kabla ya kujiunga na Persib Bandung.

michael

Michael Essien mwenye umri wa miaka 34 alikataa kujiunga  na Melbourne ya Australia mwezi December mwaka jana, Essien amewahi kuichezea Chelsea ya England kwa misimu nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *