Zaidi ya mara moja, msanii Zuwena Mohamed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Baby amewahi kuweka hadahrani kuwa yeye hajui Kiingereza cha Waingereza, yeye anaweza kuzungumza Kiingereza cha ku-unga- unga ili mradi mawasiliano yapatikane na dili la kazi lifanikiwe.

Shilole alienda mbali zaidi na kudai kuwa kuifahamu na kuimudu lugha ya Kiingereza kunahitaji BARAKA MAALUM kutoka kwa MWENYEZI MUNGU ambazo kwa kawaida huwa tunaziita KIPAJI.

Wiki hii tena ameibuka staa mpya wa kundi au lebo ya WCB, Rich Mavoko na kudai kuwa kwa sasa anajipanga ili kuwekeza nguvu kwenye kukijua vizuri Kiingereza ili asiweze kuumbuka kama ilivyowahi kumtokea miaka ya nyuma nchini Uingereza kwenye jiji la London.

Diamond Platnumz aliwahi kudai kuwa yeye hakuwa anajua kiingereza vizuri lakin akawekeza nguvu kubwa ya kuijua lugha hiyo na hivi sasa mafanikio ya jitihada hiyo yameonekana.

Je, lugha hiyo ndiyo ngazi ya kupandia wasanii ili kupata mafanikio ya kimataifa?

Wasanii wangapi wa bongo wenye uwezo mkubwa wa kuzungumza Kiingereza lakini hawaoni kuwa hiyo ni nyenzo ya kuTOBOLEA?

Au tuseme ‘MAHINDI humpata asiye na meno?’

Wasanii wa Bongo Fleva wajiulize mara mbili na watathmini kwa kina suala la matumizi ya Kiingereza na umuhimu au ulazima wake kwenye muziki wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *