Mshambuliaji wa kimtaifa wa Uganda, Emanuel Okwi uhenda akarejea Simba baada ya klabu hiyo kukubali kulipa dola za Marekani 120,000 ni zaidi ya Sh milioni 240 kwa klabu ya Sonderjiske ya Denmark ili kumrejesha msimbazi.

Baada ya klabu hiyo kukamilisha kulipa kiasi hicho cha fedha, mchezaji huyo atarejea kuichezea Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Simba ilimuuza Okwi kwa dola 100,000 mwaka juzi Denmark, lakini kutokana na mchezaji huyo kutopata nafasi ya kucheza Ulaya, imeamua kumrejesha na makubaliano yamefikiwa Sh milioni 240.

Taarifa za mitandao ya kujamii jana zilieleza kuwa, Okwi ni mchezaji aliyeipa faida kubwa Simba ndani na nje ya uwanja wakati ule akiichezea klabu hiyo ya Msimbazi.

Simba ilimuuza Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka 2013 kwa dau la rekodi kwa klabu za Tanzania, dola 300,000, ingawa baada ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia.

Mtafaruku ulianza baada ya Okwi kuchelewa kurejea mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa, Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *