Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amesema kuwa hana shida na Mume mpya wa aliyekuwa mkewe madam Flora Daudi Kusekwa.

Kauli hiyo ya Mbasha imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mke wake wa ndoa, Flora kufunga ndoa na Daudi Kusekwa mkoani Mwanza.

Mbasha amesema kuwa hana shida na  mume mpya wa Flora kwani yeye hamfahamu na kama akikutana naye hawezi kumfanya lolote maana huyo mtu hakuwahi kumuingilia katika ndoa yake.

Ndoa ya Madam Flora iliyofanyika wiki iliyopita
Ndoa ya Madam Flora iliyofanyika wiki iliyopita

Pia muimbaji huyo amesema kuwa Flora amemkimbia kutokana na maisha aliyoyachagua lakini si kwamba alikuwa hana pesa, kwani yeye pesa alikuwa nazo toka mwanzo.

Flora ambaye kwasasa anajulikana kama Madam Flora amefunguka ndoa wiki iliyopita mkoani Mwanza na mwanaume anayefahamika kwa jina la Daudi Kusekwa ambaye anaonekana kiumri mdogo kuliko Flora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *