Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal, El Hadji Diouf alipata sifa ya kuwa kijana mtukutu wakati akicheza mpira.

Kwasasa amchezaji huyo amestaafu anasema kuwa sifa yake ya utukutu haikuwa nzuri kipindi anacheza mpira.

El Hadji Diouf ni shujaa nchini Senegal na kila mahala anakokwenda hushangiliwa na mashabiki wakiwemo vijana na hata wazee.

Watu nchini Senegal bado wanamshukuru kwa wajibu aliotekeleza wakati wa kombe la dunia mwaka 2002 nchini Japan na Korea Kusini.

Lakini nchini Uingereza anakumbukwa kwa sarakasi zake uwanjani kuliko umahiri aliokuwa nao katika usakataji kandanda.

Ni tabia ililomfuata hadi kwa ligi za Uingereza alipocheza na Liverpool na Blackburn Rovers hadi Bolton Wanderes na Rangers ya Scotland.

Diouf aliwatemea mate wapinzani na kuwakabili wasimamizi wa mechi na wapinzani wakati wa mechi za klabu yake.

Diouf ambaye sasa amehamia mji mkuu wa Senegal Dakar, anasema kwa mara kadha hakueleweka vyema wakati wa siku zake akicheza England.

Alipoulizwa na mambo yapi, alisema alikuwa akiwatemea mate wapinzani labda walipomuambia kitu ambacho hakukipenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *