Mataifa ya Afrika Magharibi yaliyosaidia kuondoka madarakani kwa rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh kisha kujitolea kulinda usalama nchini Gambia yamepanga kupunguza idadi ya wanajeshi hao nchini humo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ombi la rais wa Gambia, Adama Barrow kwa Ecowas kuruhusu wanajeshi hao kusalia nchin humo kwa miezi sita zaidi.

Taarifa ya mkuu wa jeshi la Senegal linaloongoza vikosi hivyo, Jen. Francois Ndiaye imesema kuwa kwakuwa hali ya usalama imeamiarika nchini Gambia wanafikiri ni vyema kupunguza idadi ya wanajeshi waliopo nchini humo kwaajili ya kazi ya kulinda usalama.

Vikosi vitakavyopunguzwa ni pamoja na anga na maji ingawa hivyo vitapunguzwa kwa uchache sasa ikilinganishwa na askari wa ardhini.

Jen. Ndiaye alikataa kutaja idadi kamili ya wanajeshi waliopelekwa Gambia ingawa mkuu wa Ecowas, Marcel Alain de Souza, aliwahi kudai kuwa vikosi hivyo vinafikia wanajeshi 4,000 ambao ni sehemu ya wanajeshi 7,000 waliopaswa kupelekwa nchini humo.

Nchi zilizochangia wanajeshi ni pamoja na Senegal, Nigeria na Ghana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *