Mchekeshaji wa kundi la Timamu Africa, Ebitoke amesema ameamua kumuacha Ben Pol aliyekuwa akidaiwa kuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma.

Kauli ya Ebitoke inakuja mara baada ya drama za hapa na pale hivi karibuni kuwa wawili hao wamezinguana licha ya wao kutopenda kuliweka hilo wazi.

Ebitoke amesema kutokana na ubize wa Ben Pol na malengo yake ameamua kumuacha kwasababu hawezi kuumia na mtu ambaye ana mapenzi.

Pia amesema “Unajua mapenzi ni hisia, nahisi nilikuwa kama namlazimisha lakini nimegundua siwezi nikakosa furaha nikashindwa kufanya baadhi ya malengo yangu, kwa hiyo nimeamua kumuacha afanye maisha yake, ameniacha na mimi nimemuacha tu, nimeamua kutulia nifanye mambo yangu”.

Katika hatua nyingine amesema kwa sasa hawezi kuja kumtangaza mpenzi wake hadharani na kitu alichojifunza ni kukaa kimya katika maisha ya kimahusiano.

Wawili hao wanaidawa kuwa wapenzi siku za nyuma baada ya Ebitoke kueleza hisia zake za kumpenda Ben Pol licha ya watu kusema kuwa wawili hao walifanya hivyo kama kiki za kutaka umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *