Muigizaji wa vichekesho, Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’ amesema kuwa anavutiwa zaidi na Ben Pol na ndiyo mana alionesha hisia zake kwake.

Ebitoke amesema kuwa Ben Pol hakumtenga wala kumdharau kutokana na kazi yake hiyo bali alimkubali na kumuhakikishia kumpa support katika kazi yake hiyo ili afanikiwe zaidi na zaidi.

“Kuna watu wananitisha kweli wanakuja ‘DM’ wengine wananitukana, wengine hivi wewe Ebitoke unaweza kuwa na Ben Pol? Hivi mimi wananionaje hawa watu wasinichukulie poa poa.

“Tunachotarajia sasa Ben Pol kwanza lazima anipe ‘support’ kwa kila kitu nachokifanya na mimi lazima nihakikishe natimiza malengo yang.

Mbali na hilo Ebitoke amesema kuna mambo mengi yeye na Ben Pol wameyapanga na anaamini kuwa yatatimia mbele ya safari katika maisha yao ya kila siku.

Pia amesema kaka zake yeye walimjia juu kuona hizo stori za mahusiano na Ben Pol lakini baadaye walielewa kuwa anachofanya ni kutafuta maisha hivyo ilibidi wamuache na kazi yake hiyo ya uigizaji na kuendelea kumpa sapoti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *