Mchekeshaji maarufu kutokea Timamu Entertainment, Ebitoke amesema kuwa kwasasa hayupo katika mahusiano mazuri na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol.

Ebitoke amesema Ben Pol amekuwa akimpuuzia kwa mambo kadhaa hasa katika suala zima la mawasiliano kutoka na na muda mwingi kutokopkea simu yake.

Mchekeshaji huyo amesema kuwa “Simuelewi Ben Pol, simu hapokei, text hanilibu, ananipuuzia sijui kwanini” amesema Ebitoke. Hata hivyo ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa suala hilo linamuumiza sana kwani walikuwa na malengo makubwa sana.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Hawezi kunichomoka kwa sababu tulipanga kabisa malengo na nitaendelea kuyapigania,” amesema.

Amesema kuwa wakati wanaanza uhusiano wao Ben Pol alikuwa single hivyo hana wasi wasi iwapo anafanya hivyo kutokana na mahusiano aliyokuwa nayo hapo awali.

Wawili hao walitangaza kuwa katika mahusiano mwanzoni mwa mwaka huu baada ya Ebitoke kujitokeza katka mitandao ya kijamii na kutamka wazi kuwa anampenda Ben Pol.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *