Baada ya uzinduzi wa tuzo za ‘EATV Awards’ leo kampuni hiyo imetangaza vipengele vitakavyokuwepo kwenye tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Disemba 10 mwaka huu.

Tuzo hizo zitahusisha kazi za muziki na filamu zilizotoka mwaka mmoja uliopita kuanzia tarehe 1 Julai 2015 mpaka tarehe 30 Juni 2016 na zinazotambulika na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Vipengele hivyo ni

  1. Mwanamuziki bora wa kiume

2.Mwanamuziki bora wa kike

  1. Mwanamuziki bora chipukizi
  2. Kundi bora la muziki
  3. Video bora ya muziki
  4. 6.Wimbo bora wa mwaka

Kwa upande wa filamu ni

  1. Muigizaji bora wa kiume
  2. Muigizaji bora wa kike
  3. Filamu bora ya mwaka

Kipengele cha 10. ni Tuzo ya heshima ambayo itatolewa kwa mtu aliyetoa mchango wake kwenye sanaa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita.

logo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *