East Africa Television LTD leo imezindua tuzo kubwa Afrika mashariki zilizopewa jina la ‘EATV AWARDS’.

Meneja Mauzo na Masoko wa East Africa Television LTD, Bw. Roy Mbowe amesema tuzo hizo zitakuwa tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa kwa Afrika Mashariki ambazo zitaruhusu wasanii wa nchi zote za jumuia ya Afrika Mashiriki kushiriki moja kwa moja.

Meneja huyo amesema kuwa tuzo hizo ambazo zitahusisha wasanii wa filamu na muziki, zitafanyika Disemba 10 mwaka huu.

Pia amesema kwamba wasanii watakaopenda kushiriki kwenye tuzo hizo wawe wamesajiliwa na BASATA, na wataji-nominate’ wenyewe na kazi zao zilizotoka mwaka mmoja uliopita.

Kwa upande mwingine Bw. Mbowe amelishukuru Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kuwaunga mkono na kuwapa kibali.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *