Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amayaagiza mashirika ya kiserikali nchini humo kutoa dawa bure za uzazi wa mpango kwa wanawake wapatao milioni sita ambao hawana uwezo wa kuzipata.

Duterte amesema kuwa anataka kupunguza idadi ya mimba zisizotakiwa husususan ni miongoni mwa watu maskini ambao ndiyo wanaoongoza kwa kuwa na mimba za utotoni zaidi kuliko watu wenye kipato.

Utekelezwaji wa amri yake hiyo unatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa kanisa katoliki la Roma.

Rais aliyekuwa madarakani kabla ya Bwana Duterte alipigania kupitishwa kwa muswada wa matumizi zaidi ya dawa za mpango wa uzazi nchini humo .

Hata hivyo mahakama kuu iliweka marufuku ya muda dhidi ya usambazaji dawa za kupanga uzazi chini ya sheria mwaka 2015 baada ya malalamiko kutoka kwa makundi yanayopinga utoaji mimba.

Zaidi ya 80% ya Wafilipino ni wafuasi wa kanisa Katoliki la Roma, kulingana na kituo cha utafiti cha Pew.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *