Muigizaji wa Bongo movie, Daudi Michael ‘Duma’ amefunguka kwa kusema kwamba  tamthilia ya Siri ya Mtungi imemsaidia sana kwa kumpa fursa nyingi ndani na nje ya nchi kutokana na uigizaji wake ndani ya tamthilia hiyo.

Duma amesema kwamba tamthilia hiyo ambayo ilikuwa ikionyeshwa ndio iliyomfungulia njia ya mafanikio katika uigizaji.

Muigizaji huyo amesema kutokana na uigizaji ndani ya tamthilia ya Siri Mtungi ilimfanya apate dili la kuigiza katika tamthilia ya Kenya ambayo tayari imeshatoka

Pia muigizaji huyo amesema tasnia ya filamu kwa sasa inaushindani mkubwa hali ambayo inawafanya wasanii kuandaa kazi nzuri ili kuweza kufanya vizuri.

Muigizaji huyo hapo awali aliwahi kushiriki katika filamu ya ‘Money Desire’, ‘Its Too Lets’ na nyingine kibao.

Duma kwasasa anafanya vizuri na filamu yake mpya iitwayo ‘Mchongo sio’. ambayo ipo sokoni kwasasa.

Siri ya mtungi ni tamthilia iliyojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kutokana na kuelezea maisha halisi ya kitanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *