Mkongwe wa Bongo fleva, Dully Sykes amesema kwamba hupenda kusaidia wasanii ambao wana kiwango cha kati ili kujitengenezea njia katika maisha yake ya baadae ya kimuziki.

Dully Sykes amesema anapoamua kufanya collabo na wasanii wadogo hufanya hivyo kwa ajili ya maisha yake ya kesho kwenye game ili wakiwa wasanii wakubwa waweze kumshika mkono iwapo ataanguka hapo baadae.

Mkali huyo amesema huwa anawashirikisha vijana wakiwa katika kiwango cha kati kabla hawajafika juu kabisa kama alivyowashirikisha Diamond na Mr. Blue walikuwa kiwango cha kati kati kabla hawajafika viwango vyao sasa hivi.

Dully Sykes ameongeza kwa kusema kwamba anafanya hivyo kwa future yake kwa sababu anaweza akawatengeneza wakawa juu kabisa na akawategemea baadae wakiwa kama wanamuziki wakubwa wakamuokoa kaka yao.

Pia Dully Sykes amesema kuwa aliamua kumshirikisha mwanamuziki Harmonize kwenye wimbo wake wa mpya ‘Inde’ kwani anaamini Harmonize ni msanii ambaye ana kiwango kizuri kwasasa na anaweza kufika mbali kimataifa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *