Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Dully Sykes amesema kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Inde’ kufanya vizuri sasa anampango wa kuingia studio tena na kufanya collabo nyingine na msanii mwingine.

Dully Sykes amedai kwasasa kila kazi atakayoachia itakuwa ni ya kushirikiana maana ameshafanya sana kazi nyingi akiwa peke yake lakini kwasasa lazima afanye ngoma na wasanii wengine.

Dully amefanya kazi ya ‘Inde’ ambayo kwasasa inafanya vizuri akiwa ameshirikiana na Harmonize kutoka WCB.

Mbali na hilo Dully Skyes amefafanua kuwa kwasasa yeye hayupo WCB wala hajasaini mkataba na wowote na lebo hiyo bali wale ni watu wake wa karibu ambao amekuwa akishirikiana nao katika kazi.

Dully Sykes ni mwanamuziki mkongwe aliyeanza muziki wa Bongo fleva mwanzoni mwa miaka ya 2000 lakini kutokana na kipaji chake kuwa bora anaendelea kutamba hadi leo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *