Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Dully Sykes amesema kuwa bifu ya Alikiba na Diamond hawezi kumalizika kirahisi kutokana na wasanii hao kuwa na ‘fans base’ kubwa ndani na nje ya nchi.

Dully Sykes amekiri wazi kuwa ugomvi wa wasanii hao kwa sasa ni mkubwa kwani umeshatoka mpka kwa watu wa nje kwa hiyo kuumaliza kirahisi uwezi ila atatumia mbinu zake mpaka wawili hao wakawa sawa kabisa.

Pia mkali huyo amesema kuwa kwa sasa wasanii hao kupatana ni jambo gumu sana ila yeye anasubiri mpaka wasanii hao watakapokuwa na umri mkubwa kwake itakuwa ni rahisi kuwaweka chini na kumaliza tofauti zao.

Dully Skyes alizidi kutoa ufafanuzi kwa nini wasanii hao kwa sasa kupatana si jambo rahisi na kusema ugomvi wao umetoka nje mpka kwa watu wao wa karibu na mpka kwa mashabiki hivyo inahitaji muda.

Muimbaji huyo wa Inde amesema hayo kutokana na kuwa na mahusiano na wanamuziki hao waote wawili ambao walifundishwa muziki na mkali huyo kutokea pande za Ilala jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *