Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya amemtaka TID kuacha tabia ya kupiga picha zisizokuwa na maadili na kuziweka katika mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo ya Dudu Baya imekuja kufuatia siku za hivi karibuni kusambaa kwa picha za TID akiwa na mwanamke mwenye asili ya kihindi wakiwa kitandani kwa mahaba kitendo ambacho kimeibua mashabiki kujiuliza kwanini TID amefanya hivyo.

Dudu Baya amesema kuwa  T.I.D  hakupaswa kufanya mambo kama hayo kwa sababu kwanza anae mtoto mkubwa  ambae endapo atakuwa ameona picha hizo itakuwa imeleta pichambaya , lakini pia akiwa kama msanii mkongwe mambo ya kutafuta kiki kwa kupiga picha za hivyo anapaswa kuwaachia kina Gigy Money na Amber Lulu, hayo mambo yeye hayamfai tena.

Dudubabya anaongeza na kusema kuwa ingawa kwa sasa ni lazima ufanye kitu kikupe kiki lakini hayo hayafai kwa T.ID”wasanii wengi underground wanakwambia ili uweze kujulikana lazima ufanye kitu upate kiki,..lakini unapotengeneza kiki ni lazima uiangalie je iyo kiki unayoitengeneza yupo nani nyuma yako, mama yako, babako , kuna watoto wako.’

Inawezekana ndivyo wasanii wengi wanavyoamini kuwa katika kufanya muziki ili watu wakujue na upate jina basi ni lazima ufanye jambo la aibu ili uweze ku-trend katika mitandao, lakini kumbe sio kwa sababu unapaswa kwanza kuangalia heshima yako lakini pia kile unachokifanya kina athari gani kubwa zaidi ya kile unachokitafuta kwa muda huo.Wasanii wanapaswa kujifunza kitu kutokana na hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *