Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Dudu Baya amefunguka na kusema kuwa hakuna mtu wa kumpangia muda wa kunywa pombe hivyo ataendelea kunywa muda anaotaka yeye iwe asubuhi sana au mchana.

Dudu Baya amesema kuwa watu wanapoona yupo kimya wanadhani huenda amefulia na kusema yeye yupo busy na biashara nyingine na muda mwingi anakuwa hayuko Dar es Salaam lakini yuko poa na maisha yanakwenda safi.

Amesema kwa sasa maisha yake yako Mwanza na Kampala akija Dar anakuja kufanya kazi za kisanaa japo alishaamua kupotezea muziki na kufanya biashara zake mbalimbali kwa kuwa haishi kwa kutegemea mziki pekee.

Pia Dudu amesema kauli ya Darasa kuimba  kwamba ‘siyo chui, simba wala mamba ngozi yake inamtosha kujigamba’  haijamsumbua kwa kuwa Darasa ni kijana wake na ni msanii ambaye amepambana kwa muda mrefu ila kwa sasa kafanikiwa hivyo anampongeza kwa mafanikio.

Dudu Baya ni miongoni mwa wanamuziki waliofanya mapinduzi mpaka muziki kufika hapa ulipo kutokana na kazi zake kubamba masikioni mwa watu kama vile Mwanangu Huna Nidhamu, Nakupenda tu, Amri kum za Mungu na nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *